Thursday, 27 March 2014

JINSI YA KUPIKA DONATI


Mahitaji
Vijiko vya chakula 2 vya white vinegar
Gramu 480 za maziwa freshi
Vijiko 2 vya chakula vikubwa vya siagi yeyote
Yai 1, Kijiko 1-2 kidogo cha chai cha Vanilla
Gramu 480 ya unga wa ngano
Kijiko kidogo  1-2 cha baking powder
Kijiko 1 chai cha chumvi
Lita 1.5 ya mafuta kwa ajili ya kukaangia
Sukari ya unga gramu 120 kwa ajili ya kunyunyiza

Jinsi ya kuandaa
Mimina vinega kwenye maziwa, acha kwa dakika 5 hadi 10 maziwa yakatike na yawe mazito.
Katika bakuli la wastani, changanya siagi na sukari mpaka vilainike kabisa kisha endelea piga yai na vanila navyo vichanganyike vizuri kabisa.





Hakikisha unapata  muonekano safi kabisa baada ya mchanganyiko wako kua laini kisha changanya kwa kutumia mchapo unga wa ngano, baking Powder, na chumvi kisha chukua mchanganyiko wa maziwa na vinega mimina kwenye mchanganyiko huu wenye unga na siagi.

Sukuma mchanganyiko wako kisha kata miduara safi ya umbo la donati na katikati toboa pia, acha yakae katika joto la chumba kwa dakika 10 yaumuke wakati huo unasubiri yaumuke unandaa kikaango chako tayari kwa kukiweka jikoni.

Kangaa donati zako kwenye mafuta moto mpaka upate rangi nzuri ya kahawia , kumbuka kugeuzamara kwa mara ili yasiive upande mmoja tu. Toa katika kikaango na weka katika wavu ili inyonye mafuta.


Kwa kutumia unga ule ule unaweza ukatengeneza donati za mviringo  ‘donut rolls’ kisha kaanga na ukimaliza hazijapoa  zimwagie sukari ya unga zitakua tamu sana na muonekano tofauti.


 



No comments:

Post a Comment