Friday 28 March 2014

WANAUME NA UVAAJI VIATU

 Ni kati ya mavazi ambayo mara nyingi hayatiliwi maanani sana na wanaume, kama ilivyo kwa wanawake ingawa viatu vya wanaume ni aghali zaidi ya vile vya wanawake lakini je, wanaume hao wanaelewa kuwa uvaaji wa viatu huenda sambamba na mavazi yao na kuchangia waonekane watanashati?

Uchunguzi unaonyesha kuwa wanaume wengi hawatilii maanani suala la uvaaji wa viatu katika kukamilisha mavazi yao wengi wao wanadhani wanaweza kuvaa viatu vya aina na rangi yoyote wakatoka bila kujali nguo ulizovaa, shughuli wanayofanya wala hali ya hewa.

Watu wengi wanazingatia kununua tu nguo lakini si viatu. Katika hili wanaume ndio wanaonekana kuathiriwa zaidi na tabia hii, kwani mara nyingi wamekuwa wakionekana kutojali sana mitindo ya viatu.

Suala la kuwa na viatu vingi wao huona kama linamhusu zaidi mwanamke na si mwanaume. Mara nyingi huonekana kutilia mkazo masuala ya utanashati katika kutengeneza ndevu na nywele na nguo na kusahau kabisa kwenda na wakati katika mitindo ya viatu.Tena wapo ambao hawaoni tabu kuvaa viatu vya ofisini nyumbani au katika shughuli ambazo ni tofauti kabisa na mazingira ya ofisi.

Mfano, wanaume ambao ni askari utakuta ni kawaida kwao kuvaa viatu vyao vya ofisini katika sherehe au shughuli nyingine tofauti na zile za kiofisi na kusahau kuwa aina hizo za viatu vinatakiwa kuvaliwa kama sare ya kazini kwenye shughuli za shuluba.

Wataalam wa mambo ya mitindo wanashauri viatu kuvaliwa kulingana na shughuli iliyokusudiwa na wanaume wanatakiwa kuwa na viatu zaidi ya jozi nne, hii itasaidia sana kuwafanya waonekane watanashati na wenye kujua maana katika mitindo na fasheni kwa ujumla.

Kwa vazi la jeans
Suruali ya jeans huvaliwa na viatu vya rangi na aina tofauti tofauti ingawaje wataalamu wa mambo ya mitindo wanashauri kutokuvaa viatu vyenye rangi ya kuwaka sana kwani itapoteza maana.

Buti, raba, makubazi ni baadhi ya viatu vinavyoendana na jeans, hivyo ni jukumu la mvaaji kuoanisha vazi lake na shughuli anayoikusudia kufanya akiwa katika vazi hilo.

Na hakikisha viatu na jeans yako vinaendana na fulana au shati ulilovaa ili usionekane kichekesho katika tasnia ya mitindo.

Kwa nguo za kawaida
Mwanaume kama ilivyo kwa mwanamke huwa anakuwa na shuguli zake za kawaida ambazo si za kiofisi wala sherehe, hapa hulazimika kuvaa mavazi ya kawaida (casual wear).

Katika mavazi haya aina ya viatu inategemea na aina ya vazi hilo kama atakuwa amevaa pensi na fulana au kaptula na fulana unashauriwa kuvaa makubazi au hata raba na utakuwa na muonekano mzuri.

Ikiwa kama una safari fupi na upo katika vazi la pensi ndefu waweza kuvaa buti na ukaeleweka.

Kwa suruali ya kitambaa
Ikiwa utakuwa umevaa suruali ya kitambaa unashauriwa kuvaa viatu vinavyoendana na suruali hiyo mfano unaweza kuvaa kiatu cha ngozi cha kufuta, ili uonekane unayelewa mitindo unatakiwa kuhakikisha kuwa rangi ya viatu vyako inaendana na rangi ya mkanda au ya suruali yako.

Kwa kufanya hivyo utakuwa umeeleweka vizuri katika suala zima la mitindo na pia itakufanya uonekane wa kuvutia na kupendeza.

tips za uvaaji wa viatu kwa wanaume

*Jaribu kuchagua viatu vinavyoendana na suruali yako au vyenye rangi ya giza zaidi ya suruali yako.
*Unapofikiria viatu pia jaribu kufikiria kuhusu soksi hakikisha soksi zako ikiwa umevaa viatu vya kutumbukiza zinaendana na rangi za nguo ulizovaa, mfano haipendezi kuvaa viatu vyeupe na soksi nyekundu.
*Kama umevaa mkanda jitahidi rangi ya mkanda huo ifanane na viatu vyako.

*Hakikisha unakuwa na viatu na mkanda wa rangi nyeusi na vya rangi ya kahawia kwani vitu hivi kwa mujibu wa wataalamu wa mambo ya mitindo vinakubali aina nyingi za nguo. Hivyo inapendeza wanaume kuwa na vitu hivi.

*Ikiwa utavaa kaptula ya jeans au pensi tafadhali hakikisha unavaa na ‘sneakers’ au makubazi na si vinginevyo.

UTENGENEZAJI WA KOPE

Kope nazo humpendezesha mwanamke kuna aina ya rangi za kupaka kwenye kope, lakini zinatofautiana. Ni vyema ukawasiliana na wataalamu wa mambo ya urembo kwa ushauri na siyo kukurupuka. Siyo umemuona  fulani kapendeza na aina fulani ya rangi ya kwenye kope halafu na wewe ukakimbilia kupaka, utachekesha

Rangi ya mdomo nayo ni eneo lingine linalompendezesha mwanamke. Ukweli ni kwamba tunatofautiana sana midomo wazungu wanaita ‘Lips’ Kila mwanamke ana tofautiana midomo  na mwingine kwa hiyo hata rangi ya midomo nayo inakwenda sambambana aina ya lips na rangi ya ngozi ya mwili aliyo nayo mwanamke, siyo unajisiriba rangi ya mdomo halafu unaonekana kituko. Wasiliana na wataalamu wa urembo kwa ushauri zaidi.

Kucha kwa wanawake ni eneo lingine linolatakiwa kuwekwa katika unadhifu. Kuna baadhi ya wanawake unaweza kukutana nao kucha zao zimelika aidha kwa kung'atwa au kwa kuliwa na fangasi. Ipo aina fulani ya fangasi ya kwenye kucha inawashamblia san wanawake hususan kwa hapa Dar, sijui ni kutokana na maji kwa sababu ya kufua au kuosha vyombo au kitu kingine.
 Ni vyema wanawake wenye tatizo hilo kumuona  mtaalamu wa ngozi kwa msaada wa tiba. Unaweza kukutana na mwanamke kucha zake zimelika na zina sharp edges kiasi kwamba akikugusa utadhani umeguswa na msasa.
Au akishika Glasi ya Kinywaji ukiangalia kucha utadhani mkono ni wa mwanaume maana kwa jinsi kucha zake zilivyo hata hafanani nazo. Kuna kucha za bandia kama mwanamke ana matatizo ya kucha basi akazinunue kusitiri aibu.

Marashi, manukato au unyunyu kama wanavyoita vijana wa mjini ni muhimu kwa wanawake lakini ni vyema nikaweka angalizo. Haipendezi kwa mwanamke anayepulizia manukato yanayonukia sana mpaka yakawakera wengine ni vyema wanawake wakajipulizia marashi yenye staha na yasiyokera.

Ngozi ya mwanamke ni bora ‘sensitive’ sana na inaakiwa ipakwe aina ya mafuta au lotion yenye virutubisho kulingana na aina ya Ngozi. Kuna wanawake wenye Ngozi ya mafuta ‘Oil Skin’  kuna wenye Ngozi mchanganyiko na kuna wale wenye ngozi kavu (Dry Skin).
Ni vyema mwanamke kujua aina ya ngozi yake ili ajie aina ya product ya ngozi anayopaswa kutumia na siyo kwa sababu umemuona mwenzio  anapaka aina fulani ya losheni  na wewe unakimbilia kununua. Omba ushauri kwa wataalamu wa ngozi watakusaidia. Kuna baadhi ya maduka yanyouza vipodozi wanatoa msaada huo bure kabisa.

Mambo muhimu ya kuzingatia mwanamke anapojiremba

MATUMIZI MBALIMBALI YA POCHI KWA WANAWAKE

Pochi ni sehemu muhimu sana katika maisha ya mwanamke. Pochi zipo za aina nyingi, rangi, ukubwa na matumizi mbali mbali. Ni nadra sana kukutana na binti au mama anayetembea bila pochi, na kwa wengine maisha yao yote wanatembea nayo kwenye pochi.

Kuna vitu muhimu ambavyo ni lazima kila mwanamke akumbuke kutembea navyo kwenye pochi, na kuna vingine ni vyema kuwa navyo lakini sio lazima itatokana na mahitaji yako mwenyewe.

Pini, Sindano na uzi, kifungo, Dawa yoyote ambayo unaitumia na kuihitaji,Kitambulisho ,  Pedi ,Kalamu na notebook

Perfume , Lip shiner,  lip stick , Poda au Mack up, Wanja, Kitana, Leso au Tishu, Khanga au mtandio , Kadi ya benki,  Sandozi kama unavaa viatu virefu.

Thursday 27 March 2014

JINSI YA KUPIKA DONATI

Mahitaji
Vijiko vya chakula 2 vya white vinegar
Gramu 480 za maziwa freshi
Vijiko 2 vya chakula vikubwa vya siagi yeyote
Yai 1, Kijiko 1-2 kidogo cha chai cha Vanilla
Gramu 480 ya unga wa ngano
Kijiko kidogo  1-2 cha baking powder
Kijiko 1 chai cha chumvi
Lita 1.5 ya mafuta kwa ajili ya kukaangia
Sukari ya unga gramu 120 kwa ajili ya kunyunyiza

Jinsi ya kuandaa
Mimina vinega kwenye maziwa, acha kwa dakika 5 hadi 10 maziwa yakatike na yawe mazito.
Katika bakuli la wastani, changanya siagi na sukari mpaka vilainike kabisa kisha endelea piga yai na vanila navyo vichanganyike vizuri kabisa.

Hakikisha unapata  muonekano safi kabisa baada ya mchanganyiko wako kua laini kisha changanya kwa kutumia mchapo unga wa ngano, baking Powder, na chumvi kisha chukua mchanganyiko wa maziwa na vinega mimina kwenye mchanganyiko huu wenye unga na siagi.

Sukuma mchanganyiko wako kisha kata miduara safi ya umbo la donati na katikati toboa pia, acha yakae katika joto la chumba kwa dakika 10 yaumuke wakati huo unasubiri yaumuke unandaa kikaango chako tayari kwa kukiweka jikoni.

Kangaa donati zako kwenye mafuta moto mpaka upate rangi nzuri ya kahawia , kumbuka kugeuzamara kwa mara ili yasiive upande mmoja tu. Toa katika kikaango na weka katika wavu ili inyonye mafuta.

Kwa kutumia unga ule ule unaweza ukatengeneza donati za mviringo  ‘donut rolls’ kisha kaanga na ukimaliza hazijapoa  zimwagie sukari ya unga zitakua tamu sana na muonekano tofauti.

Wednesday 26 March 2014

UTUNZAJI WA NGOZI NA NYWELE

KAWAIDA Yai limekuwa na matumizi kama chakula kwa muda mrefu, wapo ambao hutumia chakula hicho kwa kukaanga, kuchemsha, kunywa likiwa bichi  au kuchanganya katika vyakula vingine mbalimbali.
Lakini pia kuna matumizi ya Yai zaidi ya chakula, kwani linauwezo mkubwa wa kurutubisha ngozi,  nywele na pia kuondoa uchovu.

Jinsi ya kufanya
Ukitaka kutumia Yai kuboresha muonekano wa ngozi na nywele zako,
Chukua Yai, changanya na asali kijiko kimoja cha chai  mafuta ya Olive Chukua mchanganyiko huo kisha pakaa usoni na shingoni, kaa nao kwa dakika kumi hadi 15, hii itasaidia kama una mashimo usoni yatokanayo na chunusi .

Pia itasaidia kulainisha ngozi yako na kuwa nyororo, mchanganyiko huu pia utasaidia kukuondolea michubuko au alama za kuungua na jua, mafuta au krimu usoni.Unaweza kutenganisha kiini cha Yai na ule ute mweupe, kisha chukua ute weka kwenye kikombe au bakuli, baada ya  hapo pigapiga ule ute  hadi uwe na mapovu kisha chukua povu,  linawe usoni au paka mwili mzima kisha liache likauke .

Baada ya hapo osha na maji ya uvuguvugu, ukifanya hivyo mara kwa mara itakusaidia kufanya ngozi yako iwe anga’avu.Kama umetoka kazini na unaonekana umechoka na unataka kutoka usiku, chukua ute wa yai na pakaa chini ya jicho na uache kwa dakika 10 hadi 15 kisha safisha, itasaidia kuondoa muonekano wa uchovu katika macho yako.

Kama unawashwa mwili mzima,  chukua ute wa yai kidogo halafu nyunyiza katika maji utakayoyaoga sambamba na sabuni ya kuogea ndani ya siku chache utaona matokeo. Mbali ya hayo pia kunywa maji mengi , kula matunda kwa wingi  na Juisi hufanya ngozi kuwa raini.

Njia nyingine ni kutumia tango katika sehemu ya kovu. Twanga tango na tumia mchanganyiko wake kupaka juu ya kovu. Husaidia kulainisha makovu na unapotumia kwa muda mrefu huondoa makovu pia.

Tuesday 25 March 2014

UPIKAJI WA BIRYAN YA KUKU

Mahitaji:
* 1 Kg Mchele Pishori (Basmati)
* 1 Kuku ikate vipande kawaida
* 1 Paket maziwa mgando
* 6 Vitunguu maji vikubwa, kata vipande round
     kubwakubwa
* 1 Tablespoon Vitunguu swaumu viliotwangwa
* 1 tablespoot Tangawizi mbichi iliotwangwa

* Malimao 2
* Papai bichi1, menya, toa mbegu, kata vipande alafu isagwe iwe chembe chembe.
* Viazi mviringo kiasi (kama vikubwa, 5 vinatosha, menya uvikate nusu
* Nyanya ziloiva, saga kwenye blender uchuje
*Tomato paste kiasi

* Mafuta ya kupikia, kiasi
* Chumvi Kiasi
* Cinnamon
* Pilipili Manga kiasi
* Karafuu kiasi
* Hiliki kiasi
* Zafarani (saffron) kiasi (iloweke katika maji ya moto nusu glass)
 
Jinsi ya kupika
1- Weka ndani ya blender Tangawizi, papai ilosagwa na kitunguu swaumu na maziwa mgando uvisage mpaka viewe mchanganyiko mzito. Weka pembeni
2- Osha kuku kisha ipake chumvi ukamulie malimao, mwagia mchanganyiko wa papai na tangawizi na vitunguu swaumu halafu weka jikoni uchemshe mpaka iive iwe laini (kama kuku ya kienyeji. ikiwa kuku ya kizungu usiichemshe sana itavurugika)
3- Saga vipande vyako vyote pamoja kisha uweke kwenye kuku ikiwa inachemka

4- Weka nyanya zilizosagwa kwenye blender na ile ya paste kwenye kuku inayochemka, ukoroge ichanganyike kwenye nyama
5- Menya vitunguu maji uvioshe uvikate. Weka sufuria jikoni uweke mafuta yachemke. Weka vitunguu maji ukaange mpaka viwe golden brown. Viipue uchuje mafuta uviweke pembeni vipoe.

6- Menya viazi mviringo uvikaange kwenye mafuta mpaka viive, ipua weak pembeni vipoe
7- Kama kuku imeiva, isikauke iwe na rojo, chuku vitunguu uliokaanga uvimimine kwenye kuku, na viazi pia, changanya, acha ichemke kiasi halafu ipua weak pembeni tayati kwa kuliwa.
8- Weka sufuria jikoni utie maji na chumvi, yakichemka tia mchele na mafuta. Pika kama wali kawaida unavyopikwa. Wali ukishaiva nyunyizia yale maji ya zafarani huku unageuza ili rangi isamba. Kama huna zafarani basi tumia food coloring ya orange. Funikia na uweke moto mdogo sana mpaka wali ukauke vizuri (hii ni kama haupalii na mkaa kwa juu.
Pia kama utapenda unaweza kuweka zabibu kavu  wakati unaweka mchele kwenye maji ya moto zinaivia humo chakula hiki unaweza kushushuia na kinywaji chochote lakini wengi wanapenda Juice ya ukwaju, embe, maji na nyinginezo.