Thursday 13 March 2014

Tofauti wa upakaji Make up.




KUNA  tofauti ya upakaji wa Make up kutokana na muda na sehemu unayokwenda.
Mimi binafsi nakubaliana kwamba kuna Make Up ya mchana na usiku, zipo tofauti na pia inachangia mazingira unayokwenda!

1:Make up ya mtu anayekwenda kazini inatakiwa iwe Simple na ionekane kiasili zaidi ‘More Natural’ na inamfaa mtu yoyote hata asiyekwenda kazini nzuri kwa mchana.


2: Make up ya kanisani tofauti na ya ‘Outing’ haitakiwi kuwa ya ming’aro mingi kiasi kwamba watu wote wanakushangaa na kukuona ni kituko.
Ya kanisani haina tofuti na ya kazini  hapa unaweza weka ‘Eye Shadow’ isiyong’ara kama hiyo.
                                                
3: Make up ya kutokea hasa usiku hapa inatofautiana na ya mchana, unapaka make up za rangi ndio zinakung’arisha usiku ila sio za kutisha ni zile zinazoendana na rangi yako kama unaenda kwenye chakula cha usiku ‘dinner’ mahali fulani kama klabu ingawa pia hata kwenye sinema.
kwa wale wapenzi wa rangi za kung'aa kama hizi mie naona zinafaa usiku peke yake.

4: Hapa ndio unaona vizuri makeup ya mchana na usiku inavyotofautiana, kuna wengine wanapenda make up ya hivi kwenye mitoko yao simpo na  ‘smart’.
Pia unaweza ukawa na foundation moja tu ila vipodozi ndio ukawa navyo vya usiku na mchana nikimaanisha kama eye shadow, brush, Lipstic.
Wakati unafanya hayo pia usisahau kuwa unapopaka make up usisahau kama rangi ya usoni na shingoni ni sawa. wengine wanakoleza makeup usoni wanasahau shingo zao.

No comments:

Post a Comment