Wednesday 26 March 2014

UTUNZAJI WA NGOZI NA NYWELE



KAWAIDA Yai limekuwa na matumizi kama chakula kwa muda mrefu, wapo ambao hutumia chakula hicho kwa kukaanga, kuchemsha, kunywa likiwa bichi  au kuchanganya katika vyakula vingine mbalimbali.
Lakini pia kuna matumizi ya Yai zaidi ya chakula, kwani linauwezo mkubwa wa kurutubisha ngozi,  nywele na pia kuondoa uchovu.




Jinsi ya kufanya
Ukitaka kutumia Yai kuboresha muonekano wa ngozi na nywele zako,
Chukua Yai, changanya na asali kijiko kimoja cha chai  mafuta ya Olive Chukua mchanganyiko huo kisha pakaa usoni na shingoni, kaa nao kwa dakika kumi hadi 15, hii itasaidia kama una mashimo usoni yatokanayo na chunusi .




Pia itasaidia kulainisha ngozi yako na kuwa nyororo, mchanganyiko huu pia utasaidia kukuondolea michubuko au alama za kuungua na jua, mafuta au krimu usoni.Unaweza kutenganisha kiini cha Yai na ule ute mweupe, kisha chukua ute weka kwenye kikombe au bakuli, baada ya  hapo pigapiga ule ute  hadi uwe na mapovu kisha chukua povu,  linawe usoni au paka mwili mzima kisha liache likauke .



Baada ya hapo osha na maji ya uvuguvugu, ukifanya hivyo mara kwa mara itakusaidia kufanya ngozi yako iwe anga’avu.Kama umetoka kazini na unaonekana umechoka na unataka kutoka usiku, chukua ute wa yai na pakaa chini ya jicho na uache kwa dakika 10 hadi 15 kisha safisha, itasaidia kuondoa muonekano wa uchovu katika macho yako.




Kama unawashwa mwili mzima,  chukua ute wa yai kidogo halafu nyunyiza katika maji utakayoyaoga sambamba na sabuni ya kuogea ndani ya siku chache utaona matokeo. Mbali ya hayo pia kunywa maji mengi , kula matunda kwa wingi  na Juisi hufanya ngozi kuwa raini.


Njia nyingine ni kutumia tango katika sehemu ya kovu. Twanga tango na tumia mchanganyiko wake kupaka juu ya kovu. Husaidia kulainisha makovu na unapotumia kwa muda mrefu huondoa makovu pia.

No comments:

Post a Comment