WENGI wetu tunashindwa kutofautisha mavazi ya sehemu husika
mfano Ofisini, michezoni, na yale ya usiku na sehemu nyinginezo leo nitagusia
vazi la ofisini kwa akina dada.
Unapotaka kuvaa vazi
,lazima uangalie vazi unalolivaa mda gani na mahala unapokwenda,siyo vazi la
kutokea usiku au la kimichezo unalivaa ofisini,utakuwa kichekesho mbele za watu
hata kwa wafanyakazi wenzio.
Mavazi ya kiofisi yanaeleweka lakini hasa kwa mwanamke basi
vaa sketi fupi au ndefu na blauzi ya heshima iliyofunika kitovu chako, au suti
ya heshima na koti na hata suruali ambayo haijakubana sana inafaa sana kwa
ofisi.
Kama utapendelea kuvaa gauni basi angalia mkao wa hilo gauni
ukoje maana mara nyingi gauni huwa halipendezi kuwa vazi la ofisini bali vazi
la jioni.
Mara nyingi mtu huvutia anapovaa sketi fupi au suti ya sketi
na suti ya suruali sambamba na viatu virefu ndiyo mavazi ya ofisini kwa akina
dada na hapo utakuwa umependeza.
No comments:
Post a Comment