Mahitaji:
* 1 Kg Mchele Pishori (Basmati)
* 1 Kuku ikate vipande kawaida
* 1 Paket maziwa mgando
* 6 Vitunguu maji vikubwa, kata
vipande round
kubwakubwa
* 1 Tablespoon Vitunguu swaumu
viliotwangwa
* 1 tablespoot Tangawizi mbichi
iliotwangwa
* Malimao 2
* Papai bichi1, menya, toa
mbegu, kata vipande alafu isagwe iwe chembe chembe.
* Viazi mviringo kiasi (kama
vikubwa, 5 vinatosha, menya uvikate nusu
* Nyanya ziloiva, saga kwenye
blender uchuje
*Tomato paste kiasi
* Mafuta ya kupikia, kiasi
* Chumvi Kiasi
* Cinnamon
* Pilipili Manga kiasi
* Karafuu kiasi
* Hiliki kiasi
* Zafarani (saffron) kiasi
(iloweke katika maji ya moto nusu glass)
Jinsi ya kupika
1- Weka ndani ya blender
Tangawizi, papai ilosagwa na kitunguu swaumu na maziwa mgando uvisage mpaka
viewe mchanganyiko mzito. Weka pembeni
2- Osha kuku kisha ipake chumvi
ukamulie malimao, mwagia mchanganyiko wa papai na tangawizi na vitunguu swaumu halafu
weka jikoni uchemshe mpaka iive iwe laini (kama kuku ya kienyeji. ikiwa kuku ya
kizungu usiichemshe sana itavurugika)
3- Saga vipande vyako vyote pamoja
kisha uweke kwenye kuku ikiwa inachemka
4- Weka nyanya zilizosagwa
kwenye blender na ile ya paste kwenye kuku inayochemka, ukoroge ichanganyike
kwenye nyama
5- Menya vitunguu maji uvioshe
uvikate. Weka sufuria jikoni uweke mafuta yachemke. Weka vitunguu maji ukaange
mpaka viwe golden brown. Viipue uchuje mafuta uviweke pembeni vipoe.
6- Menya viazi mviringo
uvikaange kwenye mafuta mpaka viive, ipua weak pembeni vipoe
7- Kama kuku imeiva, isikauke
iwe na rojo, chuku vitunguu uliokaanga uvimimine kwenye kuku, na viazi pia,
changanya, acha ichemke kiasi halafu ipua weak pembeni tayati kwa kuliwa.
8- Weka sufuria jikoni utie maji na chumvi,
yakichemka tia mchele na mafuta. Pika kama wali kawaida unavyopikwa. Wali
ukishaiva nyunyizia yale maji ya zafarani huku unageuza ili rangi isamba. Kama
huna zafarani basi tumia food coloring ya orange. Funikia na uweke moto mdogo
sana mpaka wali ukauke vizuri (hii ni kama haupalii na mkaa kwa juu.
Pia kama utapenda unaweza kuweka zabibu
kavu wakati unaweka mchele kwenye maji
ya moto zinaivia humo chakula hiki unaweza kushushuia na kinywaji chochote
lakini wengi wanapenda Juice ya ukwaju, embe, maji na nyinginezo.
No comments:
Post a Comment